

Lugha Nyingine
Kenya yazindua kampeni kuhamasisha fedha kwa ajili ya fidia ya migogoro kati ya binadamu na wanyamapori
(CRI Online) Mei 08, 2025
Kenya imezindua kampeni ya siku 19 jana Jumatano kuhamasisha fedha kwa ajili ya fidia ya migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.
Akizungumza na wanahabari mjini Nairobi, Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Rebecca Miano amesema nchi hiyo inakabiliwa na madai 20,000 ya fidia yenye thamani ya shilingi bilioni 1.36 za Kenya (dola kama milioni 10.5 za Kimarekani) zinazosubiri kulipwa.
Kwa mujibu wa Miano, kampeni hiyo ya kulipwa fidia inatarajiwa kuhusisha maeneo yenye migogoro ya wanyamapori, yakiwemo Laikipia, Narok, Taita Taveta, Kajiado na Samburu.
Amebainisha kuwa nchi hiyo imejitahidi kuweka uwiano kati ya ulinzi wa urithi wa asili na mahitaji ya jamii zinazoishi karibu na makazi ya wanyamapori.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma