

Lugha Nyingine
Mashambulizi ya droni katika Bandari ya Sudan yakwamisha usambazaji wa misaada ya kibinadamu
Msemaji msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Stephanie Tremblay amesema kuwa mashambulizi ya droni katika kituo cha misaada cha mji wa Port Sudan yanakwamisha usafirishaji wa misaada na wafanyakazi wawezeshaji usambazaji.
Bi. Stephanie ameongeza kuwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesimamisha shughuli zake za kutoa Huduma ya Misaada ya Kibinadamu kupitia Angani kuanzia Jumapili na hazitarejeshwa hadi hali itakapokuwa salama, hali ambayo inazorotesha zaidi utoaji wa msaada unaohitajika haraka.
Naibu Katibu Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu Tom Fletcher ameelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya mashambulizi hayo ya droni dhidi ya Port Sudan, akisema sheria ya kimataifa ya kibinadamu lazima iheshimiwe na huduma endelevu lazima zitolewe ili kuokoa raia na miundombinu ya kiraia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma