

Lugha Nyingine
Rais Xi atoa barua za pongezi kwa shughuli ya mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Russia
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ametoa barua za pongezi jana Jumatano kwa shughuli ya mawasiliano kati ya watu-na-watu na ya kitamaduni kati ya China na Russia ya kuadhimisha miaka 80 tangu ushindi wa Vita vya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita Vikuu vya Kizalendo vya Umoja wa Kisovieti.
Kwenye ujumbe wake huo, Rais Xi ameeleza kwamba miaka 80 iliyopita, watu wa China na watu wa Russia kwa pamoja walitoa mchango isiyofutika ya kihistoria katika ushindi wa Vita vya Dunia vya dhidi ya Ufashisti na kuanzisha urafiki mkubwa kwa damu usioweza kuvunjika, wakiweka msingi thabiti wa maendeleo ya ngazi ya juu ya uhusiano wa pande mbili.
Rais Xi amesema baada ya miaka 80, kutokana na juhudi za pamoja za pande zote mbili, uhusiano kati ya China na Russia umedhihirisha uhai mpya na kuunda mfano mpya wa uhusiano kati ya nchi kubwa.
Amesisitiza kuwa kuimarisha mawasiliano kati ya watu-na-watu na ya kitamaduni kuna umuhimu mkubwa na muono wa mbali kwa ajili ya kuimarisha maelewano, kuhimiza ujirani mwema na urafiki, na kuongeza uungaji mkono wa kijamii na wa umma mpana kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.
Rais Xi amesema anatumai vyombo vya habari vya nchi zote mbili vitashikana mikono ili kusonga mbele na jukumu la pamoja na kufanya mawasiliano kati ya watu-na-watu na ya kitamaduni ambayo yanaunganisha mioyo ya watu, ili kuingiza msukumo mpya katika maelewano na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili, kuyafanya upya maendeleo ya ushirikiano wa kimkakati wa uratibu wa pande zote kati ya China na Russia kwa zama mpya na kutoa mchango mpya kwenye ujenzi ya jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.
Shughuli hiyo imeandaliwa kwa pamoja Shirika Kuu la Utangazaji la China na Shirika Kuu la Utangazaji wa Televisheni na Redio la Russia.
Siku hiyo hiyo, Rais Vladimir Putin wa Russiapia alituma salamu za pongezi kwenye shughuli hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma