

Lugha Nyingine
Uthabiti wa Uchumi wa China Unavyoonekana katika Seti Tatu za Takwimu Kutoka Maonesho ya Canton
Maonesho ya 137 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China (Maonesho ya Canton) kwa njia ya ana kwa ana yamehitimishwa tarehe 5 Mei mjini Guangzhou, mkoani Guangdong, China. Maonesho hayo yamekuwa dirisha muhimu la kuonesha uthabiti wa biashara ya nje ya China.
Wununuzi 288,000 wa Nchi za Nje
Mtandao wa Marafiki Unazidi Kupanuka
“Maonyesho haya ya Canton yanaonekana kuwa na wageni wengi zaidi kuliko mengine yoyote,” amesema Ding Yanggang, Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wa China nchini Malaysia na Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara ya Kimataifa, ambaye pia ni mkuu wa Kampuni ya Biashara ya Sanjiang ya Malaysia. Aliongeza kuwa, amekuwa akishiriki kwenye maonesho ya Canton na baba yake tangu mwaka 1990, na hajawahi kukosa hata mara moja Maonesho hayo katika miaka 30 iliyopita.
“Maonesho yanaweza kukusanya kampuni zaidi ya 30,000 za uuzaji bidhaa nje, na zaidi ya wanunuzi 200,000 duniani. Huu ni mvuto wa Maonesho ya Canton,” amesema Ding. Ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo, kampuni za Malaysia zinaweza kuhisi kwa kina kuwa China ina mfumo kamili wa viwanda, mnyororo dhabiti wa usambazaji, na uwezo mkubwa wa uzalishaji.
Amesema kuwa kampuni za Malaysia na China zinakamilishana kwa nguvu zao za uwezo na ana matumaini kwamba kampuni za pande hizo mbili zitachangamkia fursa, kushirikiana kwa ajili ya kunufaishana, na kwa pamoja kuendana na changamoto zilizoletwa na hali ya kukosa uhakika duniani.
Makubaliano ya Mauzo ya Nje yanayokusudiwa yana thamani ya Dola Bilioni 25.44 za Marekani
Mpangilio wa soko ni wenye uanuwai zaidi
“Kwenye Maonyesho haya ya Canton tulijikita katika kupokea wanunuzi kutoka Ulaya, Amerika Kusini, na nchi zinazojenga kwa pamoja ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’. Kwa kubadilisha mpangilio ipasavyo, tumepanua masoko mapya” amesema Liang Zhaoxian, Mwenyekiti wa Kundi la Kampuni za Galanz, akiwa katika eneo la chapa maalumu la maonyesho ya Canton.
Kwa mujibu wa takwimu, thamani ya makubaliano yanayokusudiwa ya mauzo ya nje katika Maonesho ya 137 ya Canton ilifikia dola bilioni 25.44 za Marekani, ongezeko la asilimia 3 ikilinganishwa na Maonesho ya 135 ya Canton yaliyofanyika kipindi kama hicho mwaka jana. Miongoni mwa makubaliano hayo, kiasi cha muamala cha nchi washirika wa ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ kilichukua asilimia 60, kikiwa ni chanzo kikuu cha kuchochea kuongezeka kwa miamala.
Bidhaa Mpya Milioni 1.02
Bidhaa za Kijani na Zenye Kutoa Kaboni Chache Zawa Maarufu
Katika maonesho hayo, bidhaa mpya, teknolojia mpya, miundo mipya, nyenzo mpya na ufundi mpya vimeibuka kwa wingi. Bidhaa za kijani, zenye kutoa kaboni chache na zile za kisasa zilivutia macho ya wengi, na zimekuwa egemeo madhubuti kwa ajili ya kuongeza oda na kupanua soko. Kampuni za kiviwanda zimeonyesha bidhaa zaidi ya milioni 4.55 kwenye mabanda, zikiwemo bidhaa mpya milioni 1.02, bidhaa za kijani na zenye kutoa kaboni chache 880,000, na bidhaa za kisasa 320,000.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma