

Lugha Nyingine
Kiongozi wa Sudan amteua kaimu waziri mkuu
(CRI Online) Mei 02, 2025
Baraza la Utawala wa Sudan(TSC)limetoa taarifa tarehe 30 Aprili na kusema Mwenyekiti wa Baraza hilo na Amiri Jeshi Mkuu Bw. Abdel Fattah Al-Burhan, amemteua Dafallah Al-Haj Ali kuwa Waziri wa Masuala ya Baraza la Mawaziri na kukaimu nafasi ya waziri mkuu.
Taarifa hiyo imesema Bw. Al-Burhan pia amemteua Bw. Omer Mohamed Ahmed Siddiq kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Bw. Tuhami Zain Hajar Mohammed kuwa Waziri wa Elimu.
Uteuzi huo umefanyika wakati mgogoro kati ya jeshi la serikali ya Sudan (SAF) na kundi la wanamgambo wa Mwitikio wa Haraka (RSF) umesababisha vifo vya maelfu ya watu, na wengine zaidi ya milioni 15 kukimbia makazi yao, na kuifanya Sudan ikabiliwe na msukosuko mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma