

Lugha Nyingine
SADC yaanza kuondoa kikosi chake kutoka nchini DRC
(CRI Online) Mei 02, 2025
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imetoa taarifa jana Alhamisi ikisema kuwa imeanza kuondoa kikosi chake maalum nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa SADC bado inashughulikia kudumisha amani na usalama wa kikanda, na itaendelea kuunga mkono kutatua mgogoro katika sehemu ya mashariki mwa DRC kwa njia za kidiplomasia na kisiasa.
SADC ilituma kikosi hicho maalum nchini DRC mwezi Disemba 2023. Mwezi Januari mwaka huu wanajeshi kadhaa wa kikosi hicho waliuawa katika mapambano yaliyotokea mashariki mwa nchi hiyo. Tarehe 13 Machi, SADC ilitangaza kumaliza kazi za kikosi hicho, na kuanza kuondoa wanajeshi wake hatua kwa hatua.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma