

Lugha Nyingine
Uchumi unapaswa kustawi, si kushuka | Maoni ya People's Daily Online kuhusu Utozaji Kiholela wa Kodi wa Marekani 3
Bahari ya uchumi wa dunia si bwawa binafsi la yeyote. Kuweka kipaumbele kwa nchi yako mwenyewe na uwezo wa nchi yako kunaenda kinyume cha mwenendo wa nyakati.
Ikikabiliwa na changamoto za kujihami kibiashara na uamuzi wa upande mmoja, China inachagua kuchangia na dunia fursa za maendeleo zinazoletwa na ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalum wa China.
China inafuata ushirikiano wa kweli wa pande nyingi. Tangu Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lilipopendekezwa, matokeo ya ushirikiano yameendelea kunufaisha watu wa nchi zaidi ya 150 na kuwa jukwaa kubwa zaidi la ushirikiano wa kimataifa duniani; China imependekeza mpango wa ushirikiano wazi na jumuishi wa "Nchi za Kusini", kuwekeza na kukusanya dola za Kimarekani karibu bilioni 20 katika fedha za maendeleo, na kuingiza msukumo mkubwa kwenye maendeleo na ustawishaji wa "Nchi za Kusini" kwa hatua za kivitendo.
"Yadi ndogo na kuta ndefu" haziwezi kuzuia maendeleo ya China. Mwaka 2024, China ilianzisha karibu kampuni mpya 60,000 zilizowekezwa kwa mtaji wa kigeni, ongezeko la mwaka-hadi-mwaka la asilimia 9.9. Aprili 24, "Orodha Hasi ya Ufikiaji wa Soko (Toleo la 2025)" ilitolewa, na idadi ya vitu kwenye orodha hiyo imepunguzwa kutoka 151 katika toleo la 2018 hadi 106 ya sasa.
Ikiwa ni nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani, China inachangia asilimia takriban 30% ukuaji duniani kwa mwaka na ni mshirika mkuu wa kibiashara wa nchi na maeneo zaidi ya 150. Azma ya China ya kupanua ufunguaji mlango wa ngazi ya juu haitabadilika licha ya dhoruba.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma