Wataalam wa  ufundi wa kilimo wa China nchini Nigeria:  Wanaojikita katika kazi kwenye mashamba yenye matumaini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 09, 2023

Wang Xuemin (katikati) na wafanyakazi wa Nigeria Bruce (kushoto) na Beatrus (kulia) wakifanya kazi shambani. (Picha na Zhao Yanhong/Tovuti ya Gazetila Umma)

Wang Xuemin (katikati) na wafanyakazi wa Nigeria Bulus Inus (kushoto) na Bitrus Basa Salka (kulia) wakifanya kazi shambani. (Picha na Zhao Yanhong/Tovuti ya Gazeti la Umma)

Nigeria ina ardhi kubwa ya kilimo na mazingira mazuri ya asili, lakini kiwango cha maendeleo ya kilimo bado kiko nyuma kiasi. Data zilizotolewa na Kamati ya Uhimizaji wa Biashara ya China mwaka 2020 zimeonesha kuwa, Nigeria bado inahitaji kuagiza kutoka nje tani milioni 2.2 za mchele kila mwaka, na imekuwa nchi inayoagiza vyakula vyote kutoka nje kwa miaka 20 mfululizo.

Nigeria ikiwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika, umuhimu wa nafaka kwa nchi hiyo unaonekana wazi. Rais wa Nigeria Tinub alitangaza Julai 13 kwamba Nigeria imeingia katika hali ya dharura ya usalama wa nafaka na kuweka hatua za kukabiliana na athari za kupandishwa kwa bei ya nafaka kwa maisha ya watu.

Mwezi Oktoba, mwaka 2003, Wang Xuemin alikuja Nigeria kwa mara ya kwanza akiwa fundi aliyetumwa kutokana na mradi wa kilimo wa "Ushirikiano wa Kusini-Kusini" kati ya China na Nigeria. Baadaye amejikita katika kazi yake hiyo kwenye ardhi ya nchi hiyo kwa karibu miaka 20, ambaye amekuwa mtendaji na mshuhudia wa msaada wa kilimo wa China kwa Nigeria na ushirikiano wa kilimo kati ya nchi hizi mbili.

Mwandishi wa habari wa Tovuti ya Gazetila Umma Liu Ning (wa kwanza kutoka kulia) alitembea kwenye  mashamba yenye matumaini pamoja na Wang Xuemin, Bruce, na Beatrus. (Picha na Zhao Yanhong/Tovuti ya Gazetila Umma)

Mwandishi wa habari wa Tovuti ya Gazetila Umma Liu Ning (wa kwanza kutoka kulia) alitembea kwenye mashamba yenye matumaini pamoja na Wang Xuemin, Bulus Inus, na Bitrus Basa Salka. (Picha na Zhao Yanhong/Tovuti ya Gazeti la Umma)

Kutafiti upandaji wa aina mpya ya mpunga, na ongezeko la uzalishaji mazao kufikia karibu 30%

Baada ya kuja Nigeria, Wang Xuemin alieneza vyombo vya kilimo vya kimsingi vinavyotumiwa nchini China, kama vile mashine za kuvuna na kupukuta. Baada ya kufanya uzoefu kwa miezi kadhaa, kazi hiyo inasaidia wakulima kuongeza ufanisi wa kupukuta mazao ya kilimo kwa mara 5 hadi 7.

Tangu Mwaka 2008, Wang Xuemin na wenzake wameanza majaribio ya utafiti wa mbegu. Mnamo Mwaka 2017, walifanikiwa kupata mbegu bora na kupanda aina mpya ya mpunga Gawal R 1. Kwa sasa, mpunga wa aina hii umeenezwa na kupandwa nchini humo kwa zaidi ya miaka mitano, na kwa jumla kuongeza uzalishaji wa mchele nchini Nigeria kwa zaidi ya tani milioni 2, na kunufaisha wakulima wasiopungua 200,000.

Wafanyakazi wenyeji wa Kituo cha Maonyesho cha Ufundi wa Kilimo cha Nigeria walisema "Hujambo" kwa waandishi wa habari wa Tovuti ya Gazetila Umma. (Picha na Zhao Yanhong/Tovuti ya Gazetila Umma)

Wafanyakazi wenyeji wa Kituo cha Maonyesho cha Ufundi wa Kilimo cha Nigeria walisema "Hujambo" kwa waandishi wa habari wa Tovuti ya Gazetila Umma. (Picha na Zhao Yanhong/Tovuti ya Gazeti la Umma)

Kutoa mafunzo ya ufundi wa kilimo, kutimiza ndoto ya "ghala la chakula la Afrika"

Bulus Inus mwenye umri wa miaka 41, ni mmoja wa wanafunzi wengi wa Wang Xuemin. Mnamo Mwaka 2016, Bulus Inus alirudi katika maskani yake na kutoa mafunzo ya ufundi wa China kwa wanakijiji wenzake ili kuwasaidia kupata ongezeko la uzalishaji wa kilimo.

Kuanzia mwaka 2006, Kampuni ya kilimo ya kijani ya Afrika magharibi ya Kampuni ya Biashara ya China ya Ng'ambo imeshirikiana na Jimbo la Kebbi, kusaidia jimbo hilo kuwaandaa zaidi ya mafundi watano kila mwaka, hasa ni mafunzo ya ana kwa ana na kuweka mkazo katika kufanya uzoefu.

Wang Xuemin, ambaye sasa ni msaidizi wa meneja mkuu wa Kampuni ya kilimo ya kijani ya Afrika magharibi, alifahamisha kuwa hivi sasa kuna wafanyakazi wanane wa China na wafanyakazi 50 wa Nigeria katika kituo hicho cha vielelezo. Kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, kwa ufadhili wa serikali ya China na Ubalozi wa China nchini Nigeria, kituo hicho kilitoa mafunzo mara mbili kwa mafundi wa Nigeria kwa mwaka, na jumla ya watu zaidi ya 400 walipewa mafunzo.

Katika miaka kumi iliyopita, China imekuwa ikifuata wazo la kupata maendeleo kwa pamoja, na imeendelea kutoa msaada kwa nchi zinazoendelea zilizoko kwenye “Ukanda Mmoja, Njia moja”katika ujenzi wa miundombinu ya kilimo, mitaji ya kilimo, ufundi na nafaka, ili kusaidia nchi hizo kujiendeleza katika sekta ya kilimo hatua kwa hatua.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha