Mwitikio wa China katika kukabiliana na UVIKO-19 wathibitisha nguvu na uhimilivu wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2022

Mhudumu wa afya akitoa dozi ya chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa mkaazi mzee katika Kijiji cha Hufeng, huko Wenchang, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Desemba 22, 2022. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

BEIJING – Huku Mwaka Mpya ukikaribia, maduka makubwa na maeneo maalum kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa na kumbi za sinema katika Mji wa Beijing nchini China sasa zinakaribisha hali ya kuongezeka kwa wateja kwa hatua madhubuti.

Kote nchini China, njia za uzalishaji kwenye mtandao mkubwa wa viwanda wa China zimeamka, haziruhusu usumbufu wowote kwa minyororo ya ugavi. Mikoa na miji mingi ya China imetuma wajumbe wa biashara nje ya nchi ili kuimarisha uhusiano na washirika na wafanyabiashara wenzao na kutafuta fursa mpya.

Uhai huo katika uchumi wa China, ambao unakuja baada ya nchi hiyo kuboresha hatua za mwitikio wa janga, unaakisi mafanikio mapya katika juhudi thabiti za China kuratibu uzuiaji na udhibiti wa janga na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mfanyakazi akikagua ubora wa bidhaa katika kiwanda cha kutengeneza baiskeli na vitembezi vya watoto katika Wilaya ya Pingxiang, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, Desemba 27, 2022. (Xinhua/Mu Yu)

Kuyapa kipaumbele maisha ya watu

Kuweka maslahi ya watu mbele na kuyapa kipaumbele maisha ya watu imekuwa kipengele bainifu cha mapambano ya China dhidi ya janga la UVIKO-19.

Tangu kuanza kwa mlipuko wa virusi vya Korona, Serikali ya China imelinda maisha na afya ya watu katika kipindi kibaya zaidi cha virusi. Kipaumbele cha kulinda maisha ya watu kimezingatiwa katika mapambano ya nchi hiyo dhidi ya virusi.

Kwa mfano, ili kudhibiti janga hilo huko Wuhan, Mkoa wa Hubei katikati mwa China, mapema Mwaka 2020, zaidi ya madaktari 40,000 walitumwa kusaidia ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji mkubwa zaidi wa rasilimali za matibabu tangu kuanzishwa kwa China Mpya Mwaka 1949.

Picha hii iliyopigwa Januari 24, 2020, ikionyesha eneo la ujenzi wa Hospitali ya Huoshenshan huko Wuhan, Mkoa wa Hubei katikati mwa China. (Xinhua/Xiao Yijiu)

Juhudi hizo zimefanyika katika maeneo yote ya China na katika ngazi ya kimataifa ambapo China imetoa misaada mingi zaidi ya vifaa tiba na chanjo dhidi ya UVIKO-19. Hospitali ya kutibu wagonjwa wa UVIKO-19 ya Huoshenshan huko Wuhan, Mkoa wa Hubei ilijengwa katika kipindi kifupi usiku na mchana na kuvunja rekodi duniani.

Uongozi imara

Mapambano dhidi ya janga katika moja ya nchi yenye watu wengi zaidi duniani yamefanyika chini ya uongozi thabiti. Katika kukabiliwa na janga la dharura na kali Mwaka 2020, uongozi mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ulipitisha hatua za aina yake kukabiliana na "dharura ya aina yake" na mara moja ukatumia uongozi wa juu, wenye umoja thabiti.

China ilianzisha kikundi kazi cha Serikali Kuu kwa ajili ya kuratibu mwitikio wa janga hilo, ilituma timu kuu ya waelekezi huko Hubei, na kuanzisha kikosi kazi kati ya idara chini ya Baraza la Serikali la China. Jitihada hizi za kupigia mfano, zilienezwa katika mikoa na maeneo ya China, hivyo kuivusha nchi salama katika kipindi kigumu.

Hatua za kisayansi na mahsusi

Sayansi na teknolojia ni silaha zenye nguvu zaidi katika vita vya binadamu dhidi ya magonjwa.

China imetoa matoleo tisa ya mipango ya kinga na udhibiti na mipango ya uchunguzi na matibabu ili kuongoza mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Kurekebisha mikakati ili kuendana na hali iliyotokea

Ikikabiliwa na janga hilo, mwitikio wa China ulikuwa wa haraka na wenye maamuzi. Kufungwa kwa wakati kwa Wuhan kulisaidia sana kuzuia virusi kuenea. Ufuatiliaji wa haraka, upimaji, na juhudi za kuweka karantini zilisaidia kuweka kiwango cha maambukizi kuwa cha chini na kutoruhusu maambukizi yoyote mabaya ya jamii mpya za virusi vya Korona.

Katika miaka mitatu iliyopita, China imekimbia dhidi ya wakati ili kutoa chanjo, vifaa vya kupima haraka, na dawa na kupanua uwezo wa kliniki za homa. Hadi sasa inapotangaza kushusha hatari ya Virusi vya Korona, kutoka Daraja A hadi B, China imefikia hatua ya ushindi.

Jumuiya ya binadamu yenye afya

Ikikabiliana na janga la kimataifa, China ilianzisha operesheni kubwa zaidi ya dharura ya kibinadamu duniani tangu kuanzishwa kwa China Mpya, ikitoa michango katika juhudi za afya ya umma duniani.

Picha hii iliyopigwa Tarehe 28 Machi 2022 ikionyesha shehena ya chanjo dhidi ya UVIKO-19 aina ya SinoVac iliyotolewa na China katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Phnom Penh huko Phnom Penh, Cambodia. (Picha na Ly Lay/Xinhua)

China siyo tu imetoa na kusafirisha bidhaa za kukabiliana na janga hilo kwa zaidi ya nchi na maeneo 200 duniani lakini pia imesaidia zaidi ya nchi na mashirika ya kimataifa 120 kwa kutoa dozi bilioni 2.2 za chanjo dhidi ya UVIKO-19 na kutuma vikundi 38 vya wataalamu wa tiba duniani. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha