

Lugha Nyingine
Mwanadiplomasia Mwandamizi wa China akutana na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani
Yang Jiechi (wa kwanza kulia), Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, akikutana na kufanya mazungumzo na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan (wa kwanza kushoto) mjini Luxemburg, Tarehe 13 Juni 2022. (Xinhua/Ren Pengfei)
LUXEMBOURG - Yang Jiechi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Jumatatu wiki hii amekutana na kufanya mazungumzo na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan.
Pande hizo mbili zilifanya majadiliano ya dhati, ya kina, na ya kiujenzi juu ya uhusiano kati ya China na Marekani, pamoja na masuala mengine ya kufuatiliwa yenye wasiwasi wa pamoja.
Pande hizo mbili zimekubaliana kufuata maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi zao, kuongeza mawasiliano na mazungumzo, kupunguza hali ya kutoelewana na uwezekano wa kufanya makosa, na kudhibiti tofauti ipasavyo. Pia pande zote mbili zimekubaliana kwamba kudumisha njia zisizozuiliwa za mawasiliano ni muhimu na huleta manufaa.
Yang, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Kazi ya mambo ya nje ya Kamati Kuu ya CPC, ameeleza kuwa Rais wa Marekani Joe Biden amemwambia kwa mara kadhaa Rais Xi Jinping wa China kwamba Marekani haitafuti Vita Baridi vipya au hailengi kubadilisha mfumo wa China, wala haitaipinga China kupitia kuimarisha ushirikiano na washiriki wake, kuunga mkono kuifanya "Taiwan ijitenge na China," au kukusudia kutafuta mgogoro na China. Amesema upande wa China unatilia maanani sana kauli hizi.
Hata hivyo, kwa muda sasa upande wa Marekani umekuwa ukisisitiza kuzidisha kuizuia na kukandamiza China kwa njia ya pande zote. Matendo hayo, badala ya kuisaidia Marekani kutatua matatizo yake yenyewe, yameutumbukiza uhusiano wa China na Marekani katika hali ngumu sana na kuharibu kwa kiasi kikubwa mabadilishano na ushirikiano katika maeneo ya ushirikiano wa pande mbili, Yang amesema, huku akisisitiza kuwa hali kama hiyo haiakisi maslahi ya pande hizo mbili wala nchi nyingine za Dunia.
Uhusiano kati ya China na Marekani upo katika njia panda muhimu, ameweka wazi Yang, huku akisema kwamba kanuni tatu zilizopendekezwa na Rais Xi za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ni njia sahihi kwa China na Marekani katika kupatana, kwani kanuni hizo haziambatani na maslahi ya kimsingi ya Wachina na Wamarekani pekee, bali pia matakwa ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa. Zinapaswa kuwa kanuni za msingi za kuendeleza uhusiano wa China na Marekani.
Yang amesisitiza kuwa, China inachukua msimamo usio na utata na thabiti katika kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi. Amsema, Masuala ya ndani ya China hayaruhusiwi kuingiliwa na nchi nyingine, na majaribio yoyote ya kuzuia au kudhoofisha muungano wa Taifa la China yatashindwa.
Amesema, suala la Taiwan linahusu msingi wa kisiasa wa uhusianno wa China na Marekani, ambapo yasiposhughulikiwa ipasavyo, yatakuwa na athari mbaya.
“Hatari hiyo si tu ipo bali itaongezeka wakati huu ambapo Marekani inajaribu kuizuia China kwa kutumia suala la Taiwan, na kwa vile utawala wa Taiwan unaitegemea Marekani kutafuta ‘ijitenge’ kwake ” ameongeza.
Yang pia ameeleza msimamo mzito wa China kuhusu masuala yanayohusu Xinjiang, Hong Kong, Tibet, Bahari ya Kusini, pamoja na haki za binadamu na dini.
Amesisitiza kuwa upande wa Marekani unapaswa kuwa na mawasiliano mazuri na upande wa China na kufanya juhudi za pamoja katika kukuza ustawi, utulivu na maendeleo katika eneo la Asia-Pasifiki.
Pande hizo mbili pia zilibadilishana mawazo kuhusu masuala ya kimataifa na kikanda kama vile vita vya Ukraine na suala la nyuklia katika Peninsula ya Korea.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma