Tanzania yaanza kukamata swala 20 ili kuwahamishia Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 24, 2021

DAR ES SALAAM - Mamlaka ya wanyamapori nchini Tanzania imesema kwamba imeanza kukamata swala 20 ili kuwahamishia nchini Kenya.

"Ukamataji wa wanyama hao utachukua takriban siku tano kabla ya kukamilika," Allan Kijazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya simu Jumatano wiki hii.

Kijazi amesema swala wote 20 watakamatwa katika Hifadhi ya Kitaifa ya Rungwa, eneo la hifadhi katikati mwa Tanzania lenye ukubwa wa Kilomita za Mraba 9,000.

Kuhamishwa kwa swala 20 wa jamii ya roan kunatokana na makubaliano ya Desemba 10 mwaka huu ya kubadilishana swala aina ya roan na faru weusi wa kike kati ya Serikali za Tanzania na Kenya katika hatua inayolenga kuimarisha uzazi wa jamii hizo mbili za wanyama.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitoa ahadi ya kuipatia Kenya swala 20 wa roan kufuatia ombi la Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Kwa mujibu wa Rais Hassan, kwa sasa Tanzania ina takriban swala 4,000 ya aina ya roan huku Kenyaina swala 12 ya aina hiyotu.

Rais Hassan alisema Rais Kenyatta amekubali ombi la Tanzania la kuzawadia faru wawili weusi wa kike ambao watapelekwa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Hifadhi ya Ngorongoro zilizoko Kaskazini mwa Tanzania ambako kuna faru wawili weusi wa kiume, ili kuimarisha uzazi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha