Uchumi wa miezi 3 ya kwanza ya mwaka huu wa Tanzania waongezeka 4.9%

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2021

Wauzaji wanaonesha machungwa yanayosubiri kuuzwa kwenye soko la Buguruni, ambalo ni soko la vyakula vibichi huko Dar es Salaam, Tanzania. (Shirika la Habari la China Xinhua)

Jumapili benki kuu ya Tanzania ilisema kwamba, Tanzania imetimiza ongezeko la uchumi la 4.9% katika miezi 3 ya kwanza ya mwaka 2021, hii ni chini ya ongezeko la 5.9% la wakati huo huo wa mwaka 2020. Baada kamati ya sera ya fedha ilifanya mkutano tarehe 13, Sep., benki kuu ya Tanzania ilitoa taarifa ikisema kwamba, walifanya mapitio kuhusu utekelezaji wa sera ya fedha wa siku hizi na hali ya uchumi na mustakabali wa uchumi kwa jumla.

Tarehe 4, Julai, mwaka 2020, watu wanafanya manunuzi kwenye soko moja la Dar es Salaam, Tanzania. (Shirika la Habari la China Xinhua)

Taarifa ilisema kwamba, ongezeko la uchumi la 4.9% lilichangiwa na ujenzi, usafirishaji, kilimo, utengenezaji, uchimbaji wa madini, na shughuli za kuponda mawe.

Taarifa pia ilisema, maonesho ya sekta ya nje ya uchumi yanaendelea kukabiliwa na changamoto inayoletwa na COVID-19, hasa shughuli za utalii.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha