Maelezo ya pili ya picha za katuni kuhusu haki za binadamu za kimarekani
Kutumia fimbo ya vikwazo kufanya umwamba wa dhuluma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2021
Maelezo ya pili ya picha za katuni kuhusu haki za binadamu za kimarekani
Kutumia fimbo ya vikwazo kufanya umwamba wa dhuluma
Mchoraji wa picha: Lu Lingxing

Kuweka vikwazo vya upande mmoja, ni silaha muhimu inayotumiwa na Marekani kufanya dhuluma za kisiasa kwa kutegemea nafasi yake ya ubabe. Kwa muda mrefu, Marekani inaziwekea Iran, Syria, Venezuela na nchi nyingine vikwazo kwa upande wake mmoja, vikwazo hivyo vimeleta msukosuko mbaya wa ubinadamu katika nchi hizo.

Mwezi Mei, mwaka 2018, Marekani ilitangaza kwa upande wake mmoja kujitoa kutoka kwa makubaliano ya nyuklia ya Iran, na kuiwekea tena Iran vikwazo, ambavyo hata vimeongezwa. Wakati maambukizi ya virusi vya corona yanapoenea kote duniani, na hali ya janga la corona ya Mashariki ya Kati inapozidi kuwa mbaya, Marekani haijapunguza hata kidogo nguvu yake ya kuweka vikwazo, ikasababisha Iran kukumbwa na matatizo ya kununua vifaa vya mahitaji ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona, na maambukizi ya virusi vya corona yanazidiwa nchini humo, pia, wananchi wanateseka sana. Rais Rouhani wa Iran alisema, vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran ni ukandamizaji kwa watu masikini wa Iran, pia ni uvamizi dhidi ya haki za wagonjwa wa Iran.

Syria pia inasumbuliwa vibaya na vikwazo vilivyowekwa na Marekani. Mwaka 2019, Marekani ilipitisha “Sheria ya Kaisari”, na kwa kupitia silaha ya “mamlaka ya mkono mrefu” ya vikwazo vya upande wake mmoja imesababisha Syria inayoharibiwa vibaya katika vita kutoweza kupata chanzo cha fedha kutoka nje, na kuzuia vibaya maendeleo ya uchumi wa Syria. Wizara ya mambo ya nje ya Syria ilisema, hatua ya kuweka vikwazo ya serikali ya Marekani ilikwenda kinyume na sheria na kanuni za kimataifa, ni “ugaidi wa aina mpya”.

Ikichukua kisingizio cha “haki za binadamu”, inafanya kitendo cha kuvamia haki za binadamu; ikichukua kisingizio cha “usalama”, inafanya kitendo cha “Umwamba”, ikipitia kuweka vikwazo vya upande wake mmoja, inaonesha ubabe ovyo kwa nchi nyingine, na kuwadhuru vibaya watu wa nchi nyingine, Marekani inadaiwa madeni mazito ya damu kwa haki za binadmu.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha