CNN: Reli ya kasi ya China yaonesha upanuzi wa kasi na kuongezeka kwa ustawi

(CRI Online) Mei 27, 2021

CNN imeripoti kuwa, kutoka reli ya kwanza ya mwaka 2008 hadi kuwa namba moja duniani kwa kuwa na reli yenye maili nyingi, reli ya kasi ya China imeonesha nguvu ya uchumi ya nchi, upanuzi wa kasi, ukuaji wa ujuzi wa teknolojia na kuongezeka kwa ustawi.

Akinukuliwa na CNN, mtafiti kwenye taasisi ya China ya Chuo Kikuu cha London, Olivia Cheung amesema, mtandao wa reli sio tu umesaidia kuunganisha soko kubwa la taifa, lakini umeonesha maendeleo yaliyoratibiwa katika mikoa yote, ambayo ni dhana muhimu ya filosofia ya maendeleo mapya ya China.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Reli ya Taifa ya China, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2020, China ilikuwa na zaidi ya kilomita 37,900 za reli ya kasi inayofanya kazi, ambayo ni refu zaidi duniani.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha